Kuhusu Befrienders Worldwide (5)

Befrienders Worlwide ni mtandao wa kimataifa wa zaidi ya simu za msaada wa migogoro 350 zinazofanya kazi katika nchi 35 kwenye mabara 5. Shirika hili la kilimwengu linajumuisha jamii za ulimwengu zote zikiwa na ufikiaji kwa wafanyakazi wa kujitolea waliofundishwa kupatikana 24/7 kwa wale waliokata tamaa na kutaka kujiua.

Maono Yetu

Maono ya Befrienders Worldwide ni ulimwengu ambao kukata tamaa kunaweza kusuluhishwa na kuwa na vifo vichache kutokana na kujiua.

Lengo Letu

Lengo la Befrienders Worldwide ni kukuza maelewano na kuwezesha ufikiaji kwa huduma za msaada kwa watu wanaohitaji msaada wa kihisia mahali popote ulimwenguni na kuendelea kuboresha ubora wa msaada unaotolewa na vituo vya msaada na wafanyakazi wa kujitolea wa Befrienders Worldwide.